Image
Image

Cristiano Ronaldo kubakia Real Madrid hadi mwishoni mwa mismu wa 2020-2021

Mshambuliaji matata wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameongeza mkataba wake na kilabu hiyokwa miaka mitano zaidi.Leo hii tarehe 7 Novemba siku ya Jumatatu, nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kutia saini mkataba mpya utakaomwezesha kuendelea kuhudumia Real Madrid hadi tarehe 20 Juni 2021.
Kulingana maelezo yaliyotolewa na kilabu, iliarifiwa kwamba rais wa Real Madrid Florentino Perez pamoja na Ronaldo watafanya mkutano na vyombo vya habari baada ya kutia saini mkataba.
Hivi karibuni, wachezaji kadhaa wa Real Madrid pia walirefusha mikataba yao miongoni mwao wakiwemo Gareth Bale, Toni Kroos na Luka Modric watakaochezea  kilabu hiyo hadi mwaka 2022.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment