Image
Image

Mwakyembe ampa Kongole rais Magufuli.

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe, amesema Rais John Magufuli asingekuwa na ujasiri Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ungesainiwa. Ametahadharisha kuwa sasa Uingereza inaelekea kujitoa EU na tayari Burundi imewekewa vikwazo vya kiuchumi na kwamba mapungufu yako wazi ya mkataba huo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest (Chadema) alishauri wabunge waupitie mkataba na pia upande wa pili wa uzuri wa mkataba huo ujadiliwe na kuchambuliwa na wataalamu kwa Bunge na kushauri nini taifa lifanye kunufaika nao, zaidi ya kubaki kwenye ubaya pekee.
Suala la taifa lifanyeje kutokana na mkataba huo, Mbunge wa Makete, Profesa Norman Sigala (CCM), alishauri kuwepo na mwongozo kama nchi ifanye nini kuhusu mkataba huo.
Hasa katika suala la uwekezaji wa viwanda kwa bidhaa za nchi ili kutoliumiza Taifa.
Zitto: Madhara ni makubwa
Akichangia kuhusu uchambuzi huo wa wataalamu, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) alisema,"Madhara ya mkataba huu ni makubwa kuliko faida, nashauri Kamati ya Bunge (Viwanda, Biashara na Mazingira) siku chache hizi mkutane na watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara ili siku ya kujadili, mtuletee namna ya kukabiliana na changamoto tusiposaini.”
Zitto alisema kama nchi nyingine za EAC zimesaini na Tanzania haitasaini ni wazi Jumuiya ya Afrika Mashariki itavunjika na nchi ikisaini kuna changamoto nyingi hasa za kupoteza mapato, hivyo ni lazima kujadili mkataba huo kwa mapana yake na kuona namna ya kuchukua hatua.
Mkataba huo wa EPA unaozihusu nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) na Jumuiya ya Ulaya (EU), wenye vipengele 132 utajadiliwa bungeni Alhamisi wiki hii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment