Image
Image

20 wafa na 65 wajeruhiwa baada ya treni mbili kugongana Pakistan.


Watu 20 wamekufa  na 65 wamejeruhiwa baada ya treni mbili kugongana katika Mji wa bandari wa Karachi, Kusini mwa Pakistan.
Taarifa kutoka hospitali zinaeleza kuwa watu zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na baadhi yao hali zao ni mbaya.
Maafisa waandamizi  wa Mji wa Karachi wanasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na  idadi ya abiria waliokuwemo kwenye  treni hizo mbili kuwa zaidi ya Elfu-Moja.
Hiyo ni ajali ya pili  inayohusisha treni chini ya kipindi cha miezi miwili.
Ajali hiyo imetokea jriani na kituo cha treni cha Landi  wakati moja ya treni iliyokuwa ikitokea katika Mji wa Kati wa Multan ilipoigonga  kwa nyuma treni nyingine  iliyokuwa ikitokea Mji wa Lahore.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment