Image
Image

Kashfa dhidi ya Hillary Clinton yaendelea nchini Marekani.

Wapinzani wa Hillary Clinton waghadhabishwa na uamuzi wa FBI kuhusu kesi ya Hillary Clinton nchini MarekaniWakati imebakia siku moja ili kufikia tarehe 8 Novemba ambapo Marekani inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu wa rais, idara ya upelelezi ya FBI imetoa uamuzi wake kuhusiana na uchunguzi dhidi ya Hillary Clinton.
Idara ya upelelezi ya FBI ilikuwa imeanzisha uchunguzi dhidi ya Clinton kufuatia ushahidi mpya uliogundulika wa matumizi binafsi ya barua pepe za siri za serikali.
Mkuu wa FBI James Comey ametoa maelezo na kutangaza kutobadilisha uamuzi wao wala kufungua mashtaka dhidi ya mgombea huyo wa chama cha Democrats.
Kwa upande wa Clinton, wanachama wake walitoa maelezo na kufahamisha kuridhishwa na uamuzi huo baada ya kumpata mgombea huyo bila hatia.
Hata hivyo upande wa mgombea wa chama cha Republicans Donald Trump umekashifu matokeo ya uchunguzi na uamuzi huo wa FBI.
Mkuu wa usimamizi wa kampeni za Trump alisema, ''Ikiwa FBI haijabadili uamuzi wake, ina maana madai yote dhidi ya Clinton ni ya uongo.''
Mwenyekiti wa bunge la wawakilishi nchini humo Paul Ryan pia alikosoa uamuzi huo na kuikashifu FBI kwa kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya Clinton licha ya kupata ushahidi wa barua pepe za siri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment