Image
Image

Makamu wa Rais Mgeni Rasmi mkutano wa wadau wa uendelezaji wa viwanda Desemba 3.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa uendelezaji wa viwanda vya usindikaji utakaofanyika Desemba 3 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Tanzania (TAFOPA) ambao ndio waandaaji wa mkutano huo wakati wakizungumza na waandishi wa habari.
Licha ya Makamu wa Rais, viongozi mbalimbali wa serikali na binafsi wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuzindua uanzishwaji na uendelezaji wa maeneo ya viwanda vya usindikaji pamoja na kuhamasisha kutafuta washirika kutoka katika mashirika ya kimataifa ili kwa pamoja wajadiliane jinsi gani ya kuendeleza maeneo hayo ya usindikaji.
Aliongeza kuwa, chama cha wasindikaji kwa kuliona hilo wameona ni muda muafaka kwa sababu Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupitia mkutano huo utasaidia chama hicho kwa kushirikiana na wadau ili kutafuta maeneo ya usindikaji na kuwaondoa kina mama kutoka kusindika majumbani na kuwa na maeneo maalumu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment