Image
Image

Twiga Stars yainyonga Cameroon kama salome kwa kuifunga mabao 2-1.

TIMU ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imewaduwaza Wacameroon juzi baada ya kuifunga timu yao kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Omnispo mjini Younde. Huo ulikuwa mchezo wa pili uliochezwa baada ya ule wa kwanza uliochezwa siku mbili kabla, ambapo Twiga Stars walifungwa mabao 2-0.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wa Cameroon, wenyeji ilitangulia kufunga bao la kuongoza lililowekwa kimiani na Agnes Nkada kabla ya Mwanahamisi Omary kusawazisha na baadaye kufunga la ushindi.
Mchezo huo ulikuwa na lengo la kukipima kikosi hicho cha Cameroon kinachojiandaa na michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa wanawake zitakazofanyika kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 3, mwaka huu.
Tayari Cameroon iliwahi kucheza pia na Kenya na kushinda bao 1-0 kama sehemu ya maandalizi hayo. Cameroon inatarajiwa kuchuana na Misri katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa Novemba 19, kwenye uwanja huo uliopo mjini Younde, wakati Afrika Kusini iliyopo Kundi B itachuana na Zimbabwe siku hiyo.
Timu hiyo ya Cameroon ipo Kundi A pamoja na Afrika Kusini, Zimbabwe na Misri wakati Kundi B lina timu za Nigeria, Ghana, Mali na Kenya.
Twiga Stars chini ya Kocha Sebastian Nkomwa imeendelea kujiwekea rekodi bora, kwani ndio mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Chalenji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment