Urusi imetangaza kwamba itashindwa kukamilisha
maandalizi ya viwanja viwili vya kombe la dunia la FIFA 2018
vilivyotarajiwa kuwa tayari Desemba 2017.Kulingana na maelezo
yaliyotolewa, viwanja hivyo ambavyo ni Nizhniy Novgorod na Volgograd
vimebainishwa kwamba hatoweza kukamilika kwa muda unaotakiwa ambao ni
Desemba 2017.
Kamati ya maandalizi ya kombe la dunia imetoa maelezo na kuarifu matumaini yao ya kukamilishwa kwa viwanja vingine vitakavyochezewa mechi za mashindano hayo.
Urusi iliwahi kutangaza mpango wa kupunguza bajeti ya maandalizi ya kombe la dunia la FIFA 2018 kwa kiwango cha fedha ruble bilioni 3.
Mashindano ya kombe la dunia la FIFA 2018 yanatarajiwa kung’oa nanga tarehe 14 Juni 2018 nchini humo na mechi zote kuchezwa katika viwanja 11 vya soka.

0 comments:
Post a Comment