Image
Image

Darasa afunguka siri ya Muziki, azungumzia shutuma za kuiba Beart ya Saida Karoli.


Mwanamuziki wa Hip hop nchini Tanzania Shariff ThabeetDarassa (DARASSA) anayetamba na wimbo wake wa Muziki hivi sasa, amesema kuwa ukimya wake kwenye Muziki kwa Takribani miaka miwili ulikuwa ni wenye kishindo kikubwa kwani amejipanga vyema sasa kuweza kuendelea kutoa muziki mzuri wenye ubora na wenye kuvutia mashabiki.
Darassa amesema kuwa kunahaja kubwa tu kwa wasanii wa Tanzania kwa umoja wao kuhakikisha wanawashawishi watanzania na mashabiki wa muziki kwa kutengeneza nyimbo zenye ubora na uzalendo wa taifa la Tanzania ili wasiwe wanatumia muda mwingi kusikiliza muziki wa njee zaidi ili kuupa sheshima muziki wa Tanzania.
Kufuatia taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Asili Saida Karoli alilalama juu ya wimbo wa DarasSa kuwa Darassa amemuibia Biti inayo fanana na wimbo wa salome Darasa amelijibu swali hilo kwa kusema kuwa sikweli.

    “Hiyo ni Tradition fellings ambayo ipo pale, marimba zikipigwa fleva yake huwa ni ile ile ila zinabadilikaga ‘Tone’ tu na Bearts ya Muziki na Bearts ya Saida Karoli ni vitu viwili tofauti ukitaka kujua ziplay pamoja pale halafu niambie kitugani kinatoka huku na kuja huku sema utachanganywa na test ya marimba inayolia”amesema Darassa.
Akizungumzia pengine alishawahi kuwaza kutumia Bearts ya Saida Karoli, Darassa amesema hajawahi hata siku moja na wakati anatengeneza wimbo huo hajawaza pia chochote wala kufikiria kutumia Beart ya Saida Karoli.
Hatua ya Kwanza ya Wimbo wa Muziki.
Kwanza Bearts ya Muziki Darasa anasema kuwa aliikuta tu Skilitoni na ABA Ndiye valipiga hiyo Tradition kwa Feelings zake, sema wakati wamekamilisha kutengeneza mtu akawashauri kwanini wasimtafute Saida Karoli kwa sababu wimbo wa Muziki ulikuwa na Mahadhi ya Kiafrika na Saida Karoli alikuwa akiimba Mahadhi ya Kiafrika tena itakuwa kizazi cha sasa na zamani.

    “Mimi niliona ni sawa na ni Aidia nzuri tu lakini kabla hatujafikia kwenda kwa saida Karoli kumsikilizisha wimbo wetu na kumpa hiyo Aidia tayari ukawa ushaa toka wimbo wa Salome wa Diamond Platinums so tukaona kunahaja tukaiacha tu hiyo aidia kwani hatukuhofia wala kuogopa chochote kwakuwa Bearts ni Mali yetu sisi na haifanani nay a Saida Karoli.”amesema Darasa.
    Akanusha kufuta sauti ya Saida Karoli.
Katika hatua nyingine Darassa amekanusha taarifa zinazodai kuwa yeye katika wimbo wa Muziki kuna vipande ambavyo Saida Karoli aliviimba lakini akavifuta baada ya Diamond kutoa salome.

    “Kwanza mimi sijawahi kukutana na Saida Karoli kabisa kwenye Maisha yangu, sijawahi kuzungumza chochote kwenye maisha yangu, kwahiyo hakuna maongezi yeyote ambayo nimewahi kufanya na Saida Karoli.”amesema Darasa.
    Kwanini Alimshirikisha Ben Pol.
Akizungumzia sababu za Ben Pol kuwepo katika wimbo wa Muziki Darassa anasema kuwa nikutokana na Ben Poul kusikiliza DEMO ambayo mimi nimefanya akaipenda ndipo akaweka wazi kwamba anahitaji wafanye kitu kwenye huo wimbo, ndipo akaona kwamba kwakuwa Ben Pol pia ni msanii mzuri na nikatengeneza vitu vya kufanya na akafanya.
Hatua za kupeleka Muziki wake Ng’ambo ipoje?
Hata hivyo Darassa amezungumzia katika kupiga hatua kuvuka Ng’ambo amesema kuwa matarajio yake nikufanya muziki mzuri ambao utawafanya wasanii wa Mataifa mengine kuvutiwa na kazi za Tanzania tofauti wasanii kufanya muziki kwaajili ya kuwa kama flani ama kufika sehemu kama msanii flani wa nje.

    “Mimi nipo tofauti kidogo mimi naona sisi tufanye kazi ifikie steji watuchukulieje sisi huku tukiwa mtizamo wa kuwachukulia wao ndio wawe ngazi kwetu sisi, wawe wakubwa milele kwetu sisi, wawe kitu cha kwanza na sisi tufuate hatuwezi kufikia malengo yetu, mimi naota ndoto tofauti kidogo ntafanya kazi zangu kuhakikisha mataifa mengine yanahitaji kolabo kwetu kuliko sisi kuhitaji”amesema Darasa.
Kwa sasa Darassa anafanya vizuri na Wimbo wake wa Muziki huku ikionesha kuzilaza chali ngoma ambazo zilikuwa zina vuma.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment