Mabasi yaliyokuwa yamejaa watu yalikuwa yaanze kuondoka alfajiri ya leo ikiwa ni sehemu ya makubaliano na Serikali ya Syria ambayo vikosi vyake vinaudhibiti Mji wa Aleppo bada ya mapigano makali.
Kwa mujibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza, hakuna muasi au raia aliyeondoka Mashariki mwa Aleppo saa kumi-na-moja alfajiri kama ilivyotakiwa.
Wanamgambo 1,500 wamesalimisha silaha zao kwenye vitongoji vya Kusini mwa Mji Mkuu wa Syria Damascus chini ya sheria ya msamaha uliotolewa na Serikali ya Rais BASHAR al-ASSAD mapema mwaka huu .
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kiarabu la Syriam,-SANA- wapiganaji hao waliokuwa na silaha wamesalimisha silaha zao katika Kijiji cha Kanaker , kwenye Jimbo la Rif Dimashq na kupelekwa kwenye kituo cha kupewa nasaha.
Chini ya sheria hiyo watakaosalimisha silaha zao ambazo walikuwa wakimiliki kwa sababu moja au nyingine wanaweza kusamehewa.
0 comments:
Post a Comment