Waendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu -ICC- ya The Hague Uholanzi wameiomba mahakama hiyo itoe kifungo cha miaka minane jela kwa makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, JEAN-PIERRE BEMBA, aliyepatikana na hatia ya kuwahonga mashahidi wakati wa kesi yake kwenye mahakama hiyo.
Waendesha Mashitaka hao wamependekeza kifungo hiho cha miaka minane kiende pamoja nan a kifungo katika kesi yake ya msingi.
Pia wamependekeza kifuo cha miaka minane jela kwa Mwanasheria wa BEMBA, aitwaye AIME KILOLO, Meneja wake wa Sheria JEAN-JACQUES MANGENDA kifungo cha miaka saba jela,shahidi wa upnde wa utetezi, NARCISSE ARIDO, kifungo cha miaka mitano jela na Mbunge wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, FIDELE BABALA kifungo cha miaka mitatu jela.
Home
Kimataifa
Slider
Waendesha Mashtaka ICC waomba Rais wa zamani wa Kongo JEAN-PIERRE BEMBA kufungwa miaka 8 jela.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment