Image
Image

Ununuzi wa vitu mbali mbali kwaajili ya X- Mass vya Dorora.

WAKATI shamrashamra za msimu wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya zikiendelea, jijini Dar es Salaam hali ya ununuzi wa bidhaa hasa vyakula ni wa kawaida mwaka huu, ikilinganishwa na kipindi hiki, mwaka jana.
Meneja wa Mipango na Biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo, Dar es Salaam, Mrero Mgheni alisema jana kuwa mzunguko wa fedha mwaka huu, umekuwa mdogo ndio maana ununuzi wa bidhaa ni wa kawaida, kama wa vipindi visivyokuwa vya sikukuu.
Mgheni alisema jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu ununuaji wa bidhaa katika soko hilo katika kipindi cha kuelekea sikukuu hizo mbili.
Alisema kwa mwaka huu, hakuna mfumuko wa bei hasa kwa bidhaa za vyakula zinazotumika kwa wingi, ikiwemo mchele, viazi mviringo, vitunguu swaumu, vitunguu maji, nyanya, viungo pamoja na nyama sokoni hapo.
“Tangu wiki hii imeanza bei za bidhaa zimebaki vile vile tofauti na miaka mingine. Kwa mfano nyanya kilo ni shilingi 800 mpaka 1,200, sado ni shilingi 3,500 lakini kipindi kingine msimu kama huu sado huwa ni shilingi 5,000 hadi 6,000. Sijui tuangalie kesho (leo) na kesho kutwa (kesho), labda hali itabadilika,” alisema.
Aliongeza kuwa kilo moja ya karoti mpaka jana, ilikuwa sh 1,500 hadi 2,000 lakini mara nyingi kipindi cha sikukuu, kilo inakuwa ni Sh 2,500 hadi 3,000.
Viazi mpaka jana kilo ilikuwa ni Sh 1,000 na 1,200 bado havijapanda, na mchele nao hauna mabadiliko yoyote, upo kati ya Sh 1,200 hadi Sh 2,000 kila mmoja ananunua kutokana na ubora wake. Habari Leo lilishuhudia umati wa watu katika soko hilo kuwa ni wa kawaida, tofauti na miaka mingine kunakuwa na msongamano mkubwa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment