Image
Image

Maeneo mengi ya nchi kukosa umeme leo kufuatia hitilafu Ubungo.

Dar es Salaam.
Kaimu Meenja Uhusiano TANESCO nchini Tanzania Bi.Leila Muhaji (TANESCO)ametolea ufafanuzi juu ya kutokuwepo kwa umeme katika maeneo mengi ya nchi hivi leo ambapo amesema kuwa Grade ya Taifa Ubungo imepata hitilafu asubuhi ya leo hivyo wanafanya utaratibu wakuweza kutizama sababu nini zilizo sababisha.
Muhaji amelazimika kulitolea ufafanuzi suala hilo mara baada ya wananchi wengi kutoelewa nini kilichosababisha umeme kukatika asubuhi, ambapo amesema utakapo tengemaa mara baada ya kushughulikia hitilafu hiyo basi utarudi.
Kufuatia taarifa hiyo ya Tannesco yakutokuwapo kwa umeme baadhi ya wananchi waliozungumza na Tambarare Halisi asubuhi ya leo wamesema kuwa mapema asubuhi walisikia kishindo kikubwa kikiashiria kuna kitu kimebutuka,huku wengine wakihisi pengine ni Transformer ya maeneo jirani lakini gafla kila mmoja alisikika akisema umeme hakuna.
Katika maeneo mengi ya jiji ikiwamo Ofisini, kwenye Biashara mbali mbali nk, yamesikika majenereta yakifanya kazi huku wasiokuwa na majenereta wakionekana kutopendezwa na hali hiyo ya umeme kukatika kwa walichokuwa wakidai kuwa vipo vitu ambavyo vinaharibika hivyo biashara zao zitaharibika.
Aidha Tannesco imepongezwa kwa kutolea taarifa suala hilo la hitilafu ya umeme ambao unafanya nchi kuwapo gizani kwa muda ambao haujajulikana mpaka pale tatizo litakapo tatuliwa jambo ambalo inabidi watanzania wanatakiwa kuwa wapole kwa suala hili. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment