Image
Image

TANZIA:Mchezaji wa Kagera Sugar afariki, TFF yathibitisha yakiri kuupokea kwa uzito.

Kufuatia kifo cha Mchezaji wa Kagera Sugar David Burhan (Pichani)kilichotokea usiku wa kuamkia 30 January 2017,Hatimaye Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF Jamal Malinzi amethibitisha kuzipokea taarifa hizo.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter Malinzi ameonesha kuguswa na kifo cha mchezaji huyo huku akitumia ukurasa huo kuandika maneno haya kwa uthibitisho kuwa taarifa ya kifo cha mchezaji huyo ina ukweli na ameipokea"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar.Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani.alisema Malizi.
David Buruhan kipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki katika Hospital ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na Malaria, Burhani aliwahi kuichezea Mbeya City na baadaye aliweza kujiunga na Majimaji ya Songea na kuitumikia msimu mmoja.
Kupitia Mitandao ya kijamii wadau wasoka wameonekana kuguswa na kifo hicho cha mchezaji wa Kagera Sugar David Burhan huku wakituma zalamu za pole kupitia kurasa hizo za Facebook, Twitter,Instagram na WhatssAp.
Mwenyezimungu aiweke roho yake pema panapostahili.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment