Image
Image

Mafundi wa TRL wakesha wakitengeneza reli iliyoharibika na kusababisha Treni kupinduka Ruvu.

Kufuatia TRENI ya abiria ya Deluxe iliyokuwa safarini kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, kuacha njia na kusababisha mabehewa kuanguka katika Stesheni za Ngeta na Ruvu mkoani Pwani, hatimaye Mafundi wameanza kazi ilikuweka miundo mbinu hiyo katika hali ya kawaida ili shughuli zingine ziendelee.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez, alisema ajali hiyo ilihusisha mabehewa matano na kati ya hayo manne yalikuwa ya abiria na moja ni lile la breki linalokaa nyuma.
Alisema  mabehewa mawili yaliacha njia na matatu yalianguka.
Siku ya jana ya 29 January 207 Ofisi wa TRL alisema haya, “Hiyo treni ilikuwa inatokea mkoani Kigoma na ilitakiwa kufika Dar es Salaam saa 11:30 jioni, lakini muda huu (saa 10:39 jioni) tumepata taarifa kwamba imepata ajali, bado tunaendelea kufuatilia kujua kama kuna majeruhi,” alisema Maez.
Alisema tayari wahandisi na mafundi wa TRL wameelekea katika eneo ilikotokea ajali hiyo.
Alisema ilitokea saa 9:40 alasiri ambapo wapo kadhaa wamejeruhiwa na mmoja hali ni mbaya.
“Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndipo taarifa za waathirika itatolewa kwa umma,” alisema. 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment