Image
Image

Wizara ya Katiba na Sheria sasa rasmi Dodoma.

WAKATI Wizara ya Katiba na Sheria ikiingia rasmi katika ofisi zake mpya mjini Dodoma 31 January 2017  baada ya kuhamia mwishoni mwa wiki, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nayo imetangaza kuhamia mjini humo wiki mbili zijazo, huku ikiwatoa hofu watumishi wanaohamia huko kwa kuwataka kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mathew Mtigumwe 31 January 2017 aliwaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuwa suala la kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.
Alitoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu kilicholenga kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea kuhamia makao makuu ya nchi, Dodoma.
Alisema awamu ya kwanza ya uhamisho utahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia Februari 14 na 15, mwaka huu huku wengine 47 watahamia muda wowote kati ya mwezi huu na Juni mwaka huu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amezindua rasmi ofisi za wizara Dodoma na kuwataka watumishi waliohamia kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Makao Makuu ya wizara hiyo yaliyozinduliwa yapo katika Chuo Kikuu cha Dodoma na tayari watumishi wa wizara hiyo 31 wamehamia rasmi wakiongozwa na Dk Mwakyembe, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju.
Awamu ya pili ya tatu zinatarajiwa kufuata utaratibu uliowekwa na kufikia mapema mwakani, watumisho wote wa wizara hiyo watakuwa wamehamia Dodoma.
Baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa mwelekeo wa kuhamia makao makuu ya nchi kwa makatibu wakuu, manaibu wao pamoja na mawaziri na manaibu wao ifikapo Februari 28, mwaka huu, tayari wizara kadhaa zimehamia ikiwemo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyohamia wiki iliyopita.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment