Uturuki imetoa pole baada ya watu zaidi ya 10 kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea katika kituo cha ukaguzi wa kuisalama karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Mogadishu.
Aidha Uturuki imekemea vikali shambulizi hilo hasa kipindi ambacho Somalia ipo katika mchakato wa kuleta amani nchini humo.
Uturuki pia imetuma salamu za rambi rambi kwa familia za wahanga na kutakia waliojeruhiwa shifaa ya haraka .
Wakati huo huo Uturuki imefahamisha kuwa uhusiano mzuri baina yake na Somalia utaendelea huku ushirikiano baina yao dhidi ya ugaidi utaendelea .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment