Image
Image

Matumizi ya simu za kisasa (smartphones) husababisha maumivu ya shingo.

Hatuwezi kufikiria kuwa tunasababisha madhara makubwa kwa kutumia muda mrefu kwenye simu zetu za kisasa (smartphone au tablet), hasa kwa vijana waliochini ya umri wa miaka 24 ambao hawawezi kugeuza macho yao mbali na simu zao hata kwa sekunde moja.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kituo cha Afya cha Uingereza cha Simpyhealth kimedhihirisha kuwa asilimia 84 ya watu waliofanyiwa utafiti wenye umri kati ya miaka 18 na 24 walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya mgongo yanasobabishwa na matumizi ya simu, kompyuta na vifaa vingine vya umeme kwa muda mrefu hasa wanapolala.
Utafiti huo umeonyesha kuwa matumizi hayo ya muda mrefu husababisha matatizo ya kiafya, kama maumivu ya shingo (hasa kwa kuangalia simu au kucheza michezo ya kompyuta kwa muda mrefu). Pia husababisha maumivu ya kwenye mabega, mshtuko wa mishipa, na hata badae kusababisha maumivu ya uti wa mgongo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment