Image
Image

Mbowe acharuka kwa kushutumiwa uuzaji dawa za kulevya, atangaza maamuzi mazito (VIDEO)

Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni Mhe Freeman Mbowe (Pichani) amekanusha tuhuma dhidi yake zilizotolewa na mkuu wa mkoa wa dar es salaam kwamba anatumia ama kuuza dawa za kulevya.
Mbowe amesema kuwa hajawahi kuthubutu kutumia, kushirikiana na wauzaji na wala kuuza dawa hizo, ambapo kauli yake hiyo anaitoa leo ikiwa ndio siku ambayo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliamuru wafike kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwaajili ya mahojiano kuhusua suala hilo.
Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma 10 February 2017 Mbowe amesema kuwa yeye na viongozi wengine wanaunga mkono jitihada za kupambana na dawa ya kulevya nchini lakini hakubaliani na njia inayotumika kupambana na dawa  hizo kutokana na kwamba inawapa nafasi wafanyabiashara dawa wa dawa hizo kukimbia.
Mbowe pia ameliomba jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa kufuata sheria, huku akitangaza hatua ambazo atazichukua kuanzia sasa za kufungua kesi Mahakamani siku ya 13 February 2017 siku ya jumatatu.
Amesema suala la kushutumiwa kuuza ama kutumia limemdhalilisha kama kiongozi jambo ambalo sirahisi kusafishika kwa sasa, hapa anazungumza zaidi Tizama VIDEO HAPA.
Wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitaja jumla ya majina 65 ya watu wanaoshutumiwa kutumia ama kuuza dawa za kulevya wakiwamo Wasanii, Wafanya biashara wakubwa pamoja na wanasiasa, na kuwataka kufika kituo kikuu cha polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwaajili ya mahojiano.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment