Image
Image

Upekuzi wa makazi ya Rais Park wazuiwa.

Waendesha mashitaka nchini Korea Kusini wamesema watafungua kesi inayolenga kuwashinikiza wasaidizi wa Rais wa nchi hiyo aliyeshitakiwa Park Geun-hye kuacha kuzuia kufanyika upekuzi katika makazi yake rasmi. 
Waendesha mashitaka walijaribu kuingia katika eneo la makazi kwa kutumia waranti iliyotolewa wiki iliyopita kutafuta baadhi ya nyaraka zinazohusiana na kashifa ya rushwa inayomuhusisha na yeye na mshirika wake. Wasaidizi wa kiongozi huyo waliwazuia waendesha mashitaka hao wakidai kuna sheria ambayo inazuia kufanyika upekuzi katika maeneo ambayo kuna siri za serikali. 
Msemaji wa idara ya waendesha mashitaka Lee Kyu-chul amesema hii leo kuwa watafungua kesi ili kuona iwapo kuzuiwa kufanyika upekuzi katika maeneo hayo ni halali kisheria. 
Amesema anatarajia mahakama itatoa uamuzi juu ya suala hilo wiki ijayo. 
Hatua hii inakuja siku moja baada ya waendesha mashitaka kusema kuwa Park alivuruga mipango ya kuhojiwa na mamlaka husika akikasirishwa na habari hizo kusambazwa kupitia katika vyombo vya habari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment