Image
Image

Mr.Nay aachia "Muda Wetu" asema kwanza ndio moto kauwasha (Video).

Msanii wa Hip hop nchini Tanzania ambaye mara nyingi huwa anasimamia kile anachokiamini iwe kwenye kazi ama kitu kingine Mr. Nay ameachia mkwaju mmoja mkali wa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "Muda wetu", licha ya ngoma yake ya "Sijiwezi" kuendelea kufanya poa.
Mr.Nay usiku wa kuamkia leo ameachia Video ya ngoma yake hiyo kupitia acount yake ya Youtube huku akisema kuwa ameamua kuachia ngoma hiyo ya "Muda wetu" baada ya kuona soko liko kimya mnoo hakuna ngoma anayoiona inakishindo hivyo amefanya hivyo ili kuchangamsha soko. 
Amesema ngoma hiyo ameifanyia Free Nation kwenye studio yake huku akisema kuwa kwanza ndio kumekucha baada ya ngoma ya "Muda Wetu" kuiweka sokoni ambapo amesema anamikwaju inayokuja hivyo watu wakae chonjo huu ni muda wa kufanya kazi.
Kutokana na ngoma zake kuwa na kishindo kikubwa anapo toa ambapo wengi wamekuwa na hamu ya kusikia wimbo huu mpya, lakini wengine wakiogofya pengine hauna lugha chafu ndani yake na kusababisha kufungiwa na usisikike, Nay aliwaweka wazi mashabiki wake waliokuwa wanaogofya nakusema yeye hakuwahi kuimba wimbo wenye matusi pengine tu watu wamekuwa wakitafasiri tofauti ila anacho amini ngoma anayoitoa huwa ina maana na ina kishindo nakusema kuwa kwanza huwa hashindani na mtu kwenye muziki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment