Image
Image

Wanasheria waweka pingamizi dhidi ya amri ya rais Donald Trump kuhusu wahamiaji.

Wanasheria katika jimbo la Virginia nchini Marekani wameweka pingamizi dhidi ya amri ya rais Donald Trump kuhusu wahamiaji, wakidai katika mahakama ya serikali kuu kwamba hatua yake ya kupiga marufuku wasafiri kutoka mataifa saba inakwenda kinyume na katiba na ni matokeo ya chuki dhidi ya Waislamu. 
Michael Kelly, msemaji wa mwanasheria mkuu wa jimbo la Virginia kutoka chama cha Democratic, Mark Herring, alisema kesi hiyo itakayosikilizwa leo katika mahakama kuu ya shirikisho mjini Washington italeta changamoto kubwa kabisa ya jimbo hadi hivi sasa. 
Pingamizi hiyo iliyotolewa na jimbo la Virginia linakuja baada ya mahakama kuu ya rufaa mjini San Francisco jana kurejesha marufuku hiyo kwa wasafiri kutoka mataifa saba yenye Waislamu wengi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment