Image
Image

RC Dar P. Makonda aitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment