Image
Image

Rais Magufuli afungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda Ikulu.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli afungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam, Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali  na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maofisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya  makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania. 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment