Image
Image

Rais Magufuli aanza ziara ya Siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Machi, 2017ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Leo asubuhi Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani na baadaye ataelekea Mkoani Lindi.
Kesho tarehe 03 Machi, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi na keshokutwa tarehe 04 Machi, 2017 atafanya ziara yake Mkoani Mtwara.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Machi, 2017 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment