Image
Image

Makamu wa Rais awasili Iringa, kuhakikisha mfumo wa ikolojia mto Ruaha unahifadhiwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Iringa na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa huo ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais Jana 10 Aprili 2017 jioni aliwasili Mkoani Dodoma, ambapo Mara baada ya kuwasili Mjini Iringa,alisomewa taarifa ya Maendeleo ya mkoa huo na Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambayo imeelezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali mkoani humo pamoja na changamoto zinazoukabili mkoa huo.
Taarifa ambayo imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Iringa imesema kuwa leo 11 Aprili 2017 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atafungua mkutano wa kwanza wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Bonde la Mto Ruaha Mkuu unaolenga kuhakikisha mfumo wa ikolojia kwenye Mto Ruaha inahifadhiwa na kuwa endelevu.
Hadi kufika Mji Iringa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametumia usafiri wa barabara kutoka Dar es Salaam- Dodoma hadi Iringa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment