Image
Image

MONUSCO chaongezewa uwezo wazaidi ili kuimarisha amani na usalama Congo.

Kikosi maalum cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kimeongezewa uwezo zaidi ili kuimarisha amani na usalama nchini humo.
Waziri wa Tanzania wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga ameyasema hayo baada ya kushiriki kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichopitisha azimio kuhusu MONUSCO.
Mahiga amesema kikosi cha MONUSCO cha kujibu mashambulizi FIB kina wanajeshi kutoka Malawi, Tanzania na Afrika Kusini.
Na kuhusu suala la bajeti ya MONUSCO ambalo lilionekana kuwa ni tete, Balozi Mahiga amesema azimio la sasa limepunguza askari wapatao 300.
Katika kikao hicho cha Baraza la Usalama, Balozi Mahiga alihutubia kwa niaba ya Rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC yenye wanajeshi katika kikosi cha FIB.
Source:UN.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment