Image
Image

Wateule wapya wa Rais Magufuli kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo 5 April 2017 anawaapisha makatibu awakuu aliowateua 4 april 2017 Ikulu Dar es Salaam, ikiwa ni mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.
Wateule haoa ambao hivi leo wanaapisha ni, Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.
Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mwingine anayeapishwa leo ni Dkt.Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).
Bi.Maimuna Tarishi anachukua nafasi iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mwingine anayeapishwa leo ni Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt. Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizarahiyo.


Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment