Image
Image

Pole pole:Zama za wenye fedha kuhonga wanachama ili wawachague wanao wataka umekwisha.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema zama za watu wachache wenye fedha chafu kuhonga wanachama na kuweka viongozi wanaowataka, zimekwisha.
Amesema CCM sasa ni chama cha wanachama wote kama Katiba inavyosema, bila ya kujali rika wala rangi na wenye kutaka uongozi ndani ya chama kwa kutumia fedha chafu, chama hakitasita kuwachukulia hatua ikiwamo kukata majina yao. Kiongozi huyo wa CCM aliyasema hayo jana mkoani Arusha alipokutana na viongozi wa chama wa Wilaya ya Arusha kutoka kata zote 25 wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Arusha.
Aliwataka wana CCM kuwataja viongozi wanaotaka uongozi kwa kugawa fedha chafu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao. Polepole aliwataka wakazi wa Arusha kutorudia makosa yaliyojitokeza katika uchaguzi zilizopita.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment