Image
Image

Prof Lipumba amjibu Maalim Seif, asema anajiona ni Sultan katika taasisi, haambiliki na hashauriki.

Siku moja baada ya katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kusema kuwa kamwe hatamsamehe wala kukaa meza moja na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, hatimaye Lipumba amejibu mapigo.
Mapema leo Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza kwenye kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Tv amesema kuwa kinacho tatiza kutokufikiwa kwa mufaka unaoendelea ndani ya chama hicho nikutokana kutoheshimu katiba ya chama. 
"Matatizo yote msingi wake mkuu yanatokana na Katibu mkuu kutoheshimu katiba ya Chama, Katibu Mkuu anajiona ni Sultan katika taasisi, haambiliki na hashauriki.
Lipumba pia amezungumzia uamuzi wake wa kujiengua ndani ya CUF, "Nilijiuzulu tarehe 5 Agosti 2015 sababu kutokuwepo kwa Umoja ndani ya chama na Makatibu wakuu wa UKAWA. Chadema walitumia nafasi kutugawa sisi wakisema hatuna mpango na Rasilimali fedha kumsimamisha mgombea Urais. 
Baada ya kujiengua uenyekiti kutokana na mambo kadha wa kadha ndani ya CUF Prof.Lipumba arudi tena na kutaka kuwa mwenyekiti wa chanma hicho. 
"Sikuwa na nia kurudi kuwa Mwenyekiti CUF ila wanachama waliniomba nirudi na baada ya uchaguzi kumalizika na hali ya uchaguzi wa Zanzibar ikawa matokeo yamefutwa na hakuna lolote linalozungumzwa kuhusu uchaguzi huo nikampigia simu Maalim Seif kuwa kwa kawaida baada ya uchaguzi kumalizika CUF huwa iko moja walipanga mkutano nikaenda kuwaeleza kuwa uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oct. 25 matokeo yatangazwe na mshindi atangazwe"
Jana 3 Mei 2017 Katibu wa CUF Maalim Seifu alisema kuwa ni bora akae meza moja na kiongozi yeyote wa CCM lakini si Profesa Lipumba kwa sababu ni msaliti.
“Siwezi kukaa meza moja na Lipumba na siwezi kumsamehe kwa jinsi alivyotusaliti. Ni bora nikae na CCM adui kwani ninawajua kabisa ni adui lakini si msaliti Lipumba…siwezi kukaa na msaliti kamwe,” alisisitiza.
Zaidi Bonyeza hapa kuona Mahojiano ya Prof.Lipumba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment