Image
Image

Bunge la Marekani kuifuta huduma ya afya Obamacare.

Bunge la wawakilishi Marekani limepanga kupiga kura leo kufutilia mbali sheria ya huduma ya afya ya nafuu unaojulikana kama Obamacare.
Wanachama wa Republican wana imani kwamba sasa wana kura za kutosha.
Kevin McCarthy, kiongozi wa wengi bungeni amesema kwamba hatua muhimu imepigwa kuelekea kuidhinishwa mojawapo ya ahadi alizotoa rais Donald Trump wakati wa kampeni.
Kipengee kilichokarabatiwa kinachoahidi dola bilioni 8 kusaidia watu walio na magonjwa ya kitambo, kinaonekana kuwaridhisha waliokuwa na shaka.
Jitihada ya awali kufutilia mbali sheria hiyo mnamo Machi haikufaulu na ilikuwa mojawapo ya wakati mgumu wa siku mia moja za kwanza za rais Trump katika utawala.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment