Image
Image

Rais Magufuli atengua na kumteua Prof Egid Beatus Mubofu kuwa Mkurugenzi Mkuu TBS.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli (Pichani) amemteua Prof. Egid Beatus Mubofu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi.John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof.Egid Beatus Mubofu umeanza tarehe 02 Mei, 2017.
Prof.Egid Beatus Mubofu (Pichani juu hapo) aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw.Joseph Masikitiko ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Bw. Joseph P. Masikitiko aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kabla ya kutenguliwa.
Gerson Msigwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Mei, 2017

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment