Image
Image

Barua za Albert Einstein zinazoelezea maisha ya furaha zauzwa dola milioni 1.5

Barua mbili za Albert Einstein zianazoeleezea falsafa yake kuhusu kuishi maisha ya furaha, zimeuzwa kweenyr soko la mnada mjini Jerusalem kwa dola milioni 1.56.
Einstein alipeana barua hizo kwa msafirishaji mmoja wa mizigo mjini Tokyo mwaka 1922 badala ya zawadi ya pesa.
Alikuwa amesikia habari kuwa alikuwa ameshinda tuzo na kumuambia msafirishaji huyo wa mizigo kuwa, kama angekuwa na bahati baraua hizo zingekuwa na umuhimu sana.
Einstein alisema kwenye barua hizo kuwa kutimiza lengo la muda mrefu halileti fuuraha wakati wote.
Mwanafisikia huyo mzaliwa wa Ujerumani alikuwa ameshinda tuzo la Nobel la fisikia na wakati huo alikuwa ziarani nchini Japan.
Wakati msafirishaji wa mizigo alifika kwenye chumba chake Einstein hakuwa na zawadi ya pesa kumpta.
Badala yake alimpa mtu huyo ujumbe aliokuwa ameuweka sahihi yake akitumia karatasi ya hoteli ya Imperial ya mjini Tokyo. Ujumbe kwenye baru hiyo iliyokuwa imeandikwa kwa lugha ya kijerumani ulisema; "Maisha ya utulivu yataleta furaha nyingi kuliko kutafuta mafanikio na ukosefu wa utulivu unaoambatana nao."
Inaripotiwa kuwa mmoja wa wanunuzi wa barua hizo ni kutoka barani Ulaya na kwamba hangependa kutajwa jina.
Muuzaji anatajwa kuwa mpwa wa msafirishaji mizigo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment