Image
Image

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yupo ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana ANTONIO GUTERRES yupo ziarani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutathmini hali ya usalama nchini humo wakati vurugu baina ya vikundi vya wanamgambo zikiimarika.
Licha ya kukabiliwa na mvua kubwa wakazi wa Mji wa Bangui  walijitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Akiwa katika ziara yake ya siku nne Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuwa na mazungumzo  na viongozi wa siasa Mjini Bangui na pia atautembelea Mji wa  Bangassou  uliopo Kusini mwa nchi hiyo eneo ambalo limeathirika zaidi na vurugu hizo.
Bwana GUTERRES pia anatarajiwa kuwatembelea waathirika wa udhalilishaji wa jinsia uliofanywa na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Kabla ya ziara ya  Bwana  GUTERRES viongozi wa Kiislam na wa Kikristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati waliutaka Umoja wa Mataifa kuufanyia mabadiliko makubwa mfumo wake wa walinzi wa amani.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment