Image
Image

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana na Korea Kaskazini.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana vilivyo na Korea Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili.
Bw. Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, likiwemo tisho kutoka Korea Kaskazini.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge.
Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.
Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo anasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.
Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: "Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini.
Miezi miwili tu iliyopita umaarufu wake ulikuwa ukishuka kufuatia kupatikana kwenye sakata, lakini alipata mwamko mpya baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili kupitia anga ya Japan.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa muungano wa chama tawala cha Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) na chama cha Komeito ulishinda viti 312 kati ya viti 465 katika bunge la chini, ushindi unaoupa muungano huo nguvu za kubadilisha katiba.
Awali Bw. Abe alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha katiba kinachozuia vita na kupelekea kutambuliwa kwa jeshi la Japan.
Miaka miwili iliyopita Bw Abe alifanikiwa kubadilisha katiba ambayo iliruhusu wanajeshi kupigana vita nje hatua ambayo ilipingwa vikali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment