Image
Image

"Blue Pearl walikoma kulipa kodi tangu Mei,2014"


Uongozi wa Ubungo Plaza Limited umesema mpangaji wake, ambaye ni hoteli ya Blue Pearl alikoma kulipa kodi ya pango tangu Mei, 2014, ambapo Novemba 3, 2017 Mahakama ya ardhi ilitoa uamuzi na kuamuru Blue Pearl kulipa deni la Sh5.7 bilioni.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ubungo Plaza, Harun Mgude amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kushinda kesi Mahakama ya Ardhi."Blue Pearl amekuwa mpangaji wetu tangu mwaka 2006 na mkataba wake ulikuwa wa miaka 15 ambao ungeisha 2021 na alikuwa akilipa vizuri lakini tangu Mei 2014 aliacha kulipa," amesema Mgude.
Amesema kutokana hilo walikwenda kufungua kesi Mahakama ya Ardhi na Blue Pearl wameshindwa, hivyo kutakiwa kulipa au kutoka ndani ya jengo."Kama mnakumbuka tuliwahi kumtoa na akarudi kwa amri ya Mahakama ili kupisha kesi kuendelea, lakini Novemba 3,2017 kesi iliisha na ameshindwa na kutakiwa kulipa deni la Sh5.7 bilioni," amesema.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment