Image
Image

Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Tunduru.

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) ya Wilaya ya Tunduru, Abdallah Mussa kwa kushindwa kumudu majukumu yake.

Kutenguliwa kwa uteuzi wa mkurugenzi huyo leo Alhamisi Novemba 9,2017 kumefanyika siku tatu baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa wakurugenzi wengine wawili.
Taarifa ya Rebecca Kwandu, mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini katika ofisi ya Tamisemi imesema Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mussa Iyombe ndiye aliyotoa taarifa ya kutenguliwa kwa uteuzi huo leo mjini Dodoma.
Amesema kutokana na hatua hiyo, uteuzi wa mkurugenzi mwingine utafanyika baadaye.
Rais Magufuli Novemba 6,2017 alitengua uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa ya Bukoba, Erasto Mfugale na wa Halmashauri ya Bukoba, Mwamtumu Dau.
Viongozi hao walishindwa kutaja kiasi cha fedha za Mfuko wa Barabara zilizopokewa kwenye halmashauri zao walipoulizwa na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Alipoitwa mbele na kutakiwa kutaja kiasi halisi cha fedha zilizopokewa katika halmashauri kwa ajili ya mfuko huo, Mwantumu alijibu kuwa ana idara nyingi anazozisimamia hivyo isingekuwa rahisi kwake kukumbuka kila kitu, hivyo ni mpaka awepo mweka hazina. Pia, alisema hawezi kusema uongo.
Dk Magufuli katika mkutano huo alisema amewasamehe lakini baadaye Ikulu ilitoa taarifa ikieleza Rais ametengua uteuzi wao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment