Image
Image

"Nyumba za Lugumi haziuziki" aliyetangazwa kuzinunua adaiwa tapeli.

Mnunuzi nyumba za Lugumi Dk Louis Shika aliyetangazwa kununua nyumba za Mfanyabiashara mkubwa Lugumi zilizopo Mbweni jijini Dar es Salaam kwenye mnada uliyofanyika leo Novemba 9,2017 amekamatwa na polisi kwa kile kinachoelezwa kuharibu mnada huo kwa kushindwa kutoa asilimia 25 ya gharama za nyumba hizo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono ambayo ndio iliyoendesha mnada huo, Scolastica Kevela amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mnunuzi huyo alipotakiwa kutoa kiasi cha fedha 'kitanguliza malipo' hakuwa na fedha hizo huku akidai zinatoka Kenya."Ni kweli tumempeleka polisi, tulimwambia atoe asilimia 25 ya mwanzo kama ambavyo sheria inataka akawa hana.. na kudai hela hiyo inatoka Kenya tusubiri leo au kesho, wakati masharti hayasemi hivyo na tulimtangazia kabla ya mnada, inaonekana hakujiandaa tukaamua tumpeleke polisi kwa kuaribu mnada", amesema Kevela
Mnada wa nyumba hizo umelazimika kurudiwa upya ili kuweza kupata mnunuzi halali wa mali za Lugumi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment