Image
Image

"Mnangagwa kuapishwa ili kumrithi Mugabe Zimbabwe"



Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, anaweza kuapishwa kama rais katika kipindi cha saa chache zijazo, kimesema chama tawala.
Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini, kulingana na Zanu-PF.
Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.
Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.
Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane.
Katika barua hiyo , Bwana Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu ukabidhianaji wa mamlaka wa amani, na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment