Image
Image

Mwongozo wa msamaha wa matibabu kwa watu wenye ulemvu kuandaliwa.

Serikali imesema inaandaa mwongozo wa msamaha wa matibabu kwa watu  wenye ulemvu wakiwemo watu wenye Ualbino.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Vijana ,Ajira na Walemavu Mh Stella Ikupa wakati akijibu swali la Mh Mgeni  Kadida mbunge wa viti maalum ambaye alitaka kujua kama serikali ipo tayari kuondoa kodi katika mafuta ya ngozi kwa watu wenye Ualibino.
Mh Ikupa amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye  Ualbino na imechukua hatua kadhaa ikiwemo kusambaza vifaa  mbalimbali vinavyotumiwa na watu wenye Ualbino.
Akaongeza kuwa katika mwaka 2016/2017 serikali kupitia Wizara ya  Elimu Sayansi na Teknlojia na Elimu ya Ufundi imesambaza miwani  ya  jua.
Aidha Mh Ikupa akasema kuwa tayari BohariKuu ya Dawa Nchini MSD imejumuisha katika orodha ya madawa,mafuta kinga kwa ajili ya kuzuia miale ya jua kwa watu wenye Ualibino.
Naibu Waziri akaongeza kuwa mafuta hayo hutolewa bure bila ya malipo  katika hospital za serikali hapa nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment