Image
Image

Rekodi waliokufa na COVID-19 yahofiwa kufikia watu zaidi ya milioni 18.

Zaidi ya watu milioni 18 - mara tatu zaidi ya rekodi rasmi zinaonyesha - labda wamekufa kwa sababu ya Covid, watafiti wanasema.

Ripoti yao inakuja miaka miwili hadi siku tangu Shirika la Afya Ulimwenguni lilipotangaza janga hilo kwa mara ya kwanza.

Timu inayochunguza vifo vya ziada vilivyotokana na Covid-19 katika Chuo Kikuu cha Washington cha Marekani kiliziangazia nchi na maeneo 191 kwa kile wanachokiita idadi ya kweli ya vifo ulimwenguni.

Vifo vingine vilitokana na virusi, wakati vingine vilihusishwa na maambukizi.

Hii ni kwa sababu kuambukizwa Covid kunaweza kuzidisha hali zingine za matibabu zilizokuwepo, kama vile ugonjwa wa moyo au mapafu, kwa mfano.

Kipimo kilichotumiwa kinaitwa vifo vya ziada - ni watu wangapi wamekuwa wakifa kuliko inavyotarajiwa ikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni, kabla ya janga hilo kukumba.

Ili kukokotoa hili, watafiti walikusanya data kupitia utafutaji wa tovuti mbalimbali za serikali, Hifadhidata ya Vifo vya Dunia, Hifadhidata ya Vifo vya Binadamu, na Ofisi ya Takwimu ya Ulaya.

Viwango vya vifo vilivyokithiri vinakadiriwa kutofautiana sana kulingana na nchi na eneo, lakini kiwango cha jumla cha kimataifa kilichohesabiwa katika utafiti huo ni vifo 120 kwa kila watu 100,000.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment