Image
Image

ZUIO LA UVAAJI BARAKOA LAONDOLEWA KENYA

Wizara ya Afya ya Kenya imeondoa agizo la ulazima wa nchi nzima kuvaa barakoa ikiwa ni mwongozo uliorekebishwa na kutolewa hii leo.

Katika agizo hilo jipya, Kagwe amesema karantini ya lazima, na kutengwa kwa kesi zilizothibitishwa za Covid-19 kumesimamishwa mara moja, na kuongeza kuwa wagonjwa wasio na dalili pia hawatahitaji kutengwa.

Aidha, ukomo wa idadi ya watu katika maeneo ya kuabudu kwa wale waliopata chanjo pia imeondolewa, Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema.

Uchunguzi wa joto la lazima na uvaaji wa barakoa katika maeneo ya wazi na ya umma pia umeondolewa, isipokuwa kwa mikusanyiko ya ndani.

Hatua hii inafuatia kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya Covid-19 na visa vikali nchini.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema viwango vya kuthibitisha kuwa na Covid-19 vimesalia chini ya 5% kwa mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo waziri huyo wa afya amehamasisha umuhimu wa kuvaa barakoa na kuendeleza hatua ya kutokaribiana. Pia amesema kuwa hatua ya kuwekwa karantini itasitishwa.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment