Image
Image

WAGENI WAMIMINIKA MABANDA YA TANZANIA YA MAONESHO YA KILIMO QATAR

 

NEMC pamoja na washiriki wengine kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) wameshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutimiza majukumu yao ya GAPEX ( General Agricultural Produce Export) ambalo ndo jukumu kuu la Bodi katika kutangaza nafaka na mazao mchanganyiko kwenye masoko ya nje.

Diana Fatukubonye ni Export Manager kutoka Bodi ya Kahawa (TCB).Bodi ya kahawa ni Shirika la umma lenye mamlaka ya kusimamia tansia ya kahawa nchini Tanzania.Uzalishaji wa kahawa kwa sasahivi ni tani 75,000 ya kahawa safi na tuko kwenye mkakati wa kuongeza uzalishaji kufika tani 300,000 mwaka 2025 .
Johnson Elibarick Kaaya ni mtaalam wa kilimo kutoka Taasisi ya Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya korosho ni taasisi ya umma iliyoanzishwa chini ya sheria 18 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010 yenye jukumu ya kusimamia tasnia zima ya maendeleo ya zao la korosho nchini Tanzania.

 






Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment