UMOJA
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama
hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na
Mkewe juu ya Rais Kikwete.
Matamko
hayo yalitolewa na Wenyeviti hao katika Mkutano na Vyombo vya habari
uliofanyika katika Ofisi za UVCCM Mkoa wa Mbeya, ambapo walisema kamwe hawawezi
kufumbia macho maneno ya uzushi na uchonganishi kati ya Serikali na wananchi.
Akisoma
tamko Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana
hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete na Dk Slaa
anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani.
Alisema
katika Mkutano alioufanya Mei 12, Mwaka huu Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya Dk.
Slaa akihutubia wananchi kuwa Raisi Kikwete ni Freemason, Mdini, Mawaziri
hawamsaidii pia ni Mafisadi na kuongeza kuwa ana ushahidi wa Cd ambazo
Raisi Kikwete akihamasisha udini na kuhusu uchinjaji.
Alisema
maneno ya Dk. Slaa ni uzushi ambao unalengo la kufitinisha Watanzania na
Serikali ya Chama cha Mapinduzi hususani anapofanya mikutano ya Hadhara katika
Mkoa wa Mbeya ambapo aliongeza kuwa Ufisadi anaousema yeye kwa Mawaziri wa Ccm ili
hali yeye mwenyewe anaongoza kwa ubadhilifu wa fedha za Wananchi.
Alitolea
mfano wa ubadhilifu uliofanywa na Chadema mkoani Mbeya kuwa ni pamoja na
Kitendo chaMwenyekiti wao Freemani Mbowe kuchangisha fedha Milioni Tatu kwa
wananchi kwa kile alichodai zingetumika kununulia maji na matibabu wakati wa
maandamano lakini hazikufanya kazi hiyo na hazijulikani zilipo.
Kajuna
alisema mbali na fedha hizo kutokujulikana matumizi yake pia Dk. Slaa
alichangisha fedha zingine Shilingi Laki saba kwa ajili ya posho ya Wabunge
waliofukuzwa bungeni jambo ambalo lilileta sintofahamu kwa wakazi wa Jiji la
Mbeya.
Alisema
ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Chadema ambao kila Mwezi wanapata ruzuku ya
takribani Milion mia Tatu lakini hawajawahi kujenga hata chumba kimoja cha
Zahanati wala kutoa msaada kwa wananchi wasiojiweza lakini wao wanazidi
kuwachangisha wananchi.
“
Jamani watanzania fungukeni muone huyu kiongozi wa namna gani Mlafi, Mchoyo na
mchochezi asiyependa kuona amani ya Nchi ikistawi” alisema Kajuna.
Aliongeza
kuwa pamoja na Chadema kupata fedha zote hizo bado zinaishia mikononi mwa watu
wachache hususani Dar Es Salaam ambapo Mikoani hawazipati na ndiyo sababu Ofisi
za Chadema Mkoa wa Mbeya zilifungwa kutokana na kutolipia pango la Nyumba deni
la Shilingi Laki tatu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Uwt Prisila Mbwaga alisema kama Wanawake wa Chama cha
Mapinduzi hawako tayari kuona matusi yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine
Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete kwamba anachangia kuibomoa Nchi.
Alisema
Shumbusho alinukuliwa akitoa matusi makubwa dhidi ya Mama Salma katika mkutano
wa hadhara uliofanyika Wilayani Mbozi akisema ameshindwa kumshauri raisi kuhusu
uongozi na namna ya kuongoza nchi.
Aliongeza
kuwa katika matusi yake alimtuhumu Mke wa Raisi kuwa ni Mwanamke Mpumbavu
anayeibomoa nchi nyumba yake kwa mikono yake Mwenyewe kama Biblia inavyosema na
kwamba yeye atakuwa tayari kumshauri Dk. Slaa atakapokuwa Raisi mwaka 2015.
Kutokana
na tuhuma hizo Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya wamemtaka
Mke wa Dk. Slaa kuacha tabia ya kumsema vibaya Mama Salma na akiendelea hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Picha
na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment