|
ZAIDI
ya wanafunzi 500 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule
mbali mbali za Sekondari Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wameshindwa kuripoti
Mashuleni kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kujiingiza katika biashara
za uchimbaji wa Madini na Uvuvi.
Kutokana
na hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro, amewataka Wazazi wa
Wanafunzi hao kuhakikisha wanawapeleka watoto wao Shuleni haraka kabla ya
kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa mzazi atakayekaidi agizo hilo.
Kinawiro
aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha
Majengo kata ya Sangambi Wilayani humo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
Afisa elimu wa Wilaya kuhusu kukithiri kwa utoro wa wanafunzi mashuleni,
Hivyo kuifanya Serikali kushindwa kufikia malengo yake ya kufuta ujinga
miongoni mwa wananchi.
Alisema
Wilaya ya Chunya inakabiliwa na Wimbi kubwa la wafugaji wenye tabia ya
kuhamahama jambo ambalo husababisha kuwakatisha masomo wanafunzi ili hali
wengine wakijikita kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na uvuvi katika
Ziwa Rukwa.
Alisema
kufikia Mwishoni mwa mwezi huu mzazi yeyote ambaye hatampeleka Mwanaye Shule
bila kujali kisingizio cha aina yoyote atakamatwa na kufikishwa mahakamani
kujibu mashtaka ya kumwachisha masomo mwanafunzi na kumpatia ajira kinyume
cha Sheria.
Mkuu
huyo wa Wilaya alisema Idadi ya watoto 500 ni kubwa sana hivyo hali hiyo
ikiachwa itazalisha Wajinga wengi jambo ambalo litakuwa mzigo kwa taifa
kutokana na wengine kuwa majambazi baada ya kukosa fedha kutokana na ajira
walizojiingiza katika umri mdogo na kukwamisha juhudi za Serikali za kujenga
Shule katika kila kata.
Kinawiro
alisema Wilaya ya Chunya kitaaluma inafanya Vizuri katika ngazi ya Mkoa
ukilinganisha na Wilaya zingine hivyo hayuko tayari kuona sifa hiyo inapotea
kutokana na wazazi wachache kuzembea na kutokujua umuhimu wa kumsomesha
mtoto, na kuongeza kuwa Halmashauri inaunga mkono juhudi za Serikali kwa kuimarisha
ujenzi wa Mabweni ili kuhakikisha watoto wa kike hawakatizwi masomo kutokana
na mimba zisizotarajiwa.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wafugaji wote waliohamia Wilayani
Chunya kinyume cha Sheria kuondoka mara moja na atakae kaidi agizo hilo
atakumbana na Operesheni kubwa ya kuwaondoa kwa nguvu ambapo kwa sasa
wanafanya doria kwa kutumia ndege maalumu ili kuwabaini wahamiaji hao.
Alisema
zoezi hilo litafanyika hivi karibuni baada ya kumalizi kuwabaini wafugaji
waliovamia misitu na sehemu za hifadhi ambapo wanaharibu kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya mifugo ambayo huharibu mazingira ya Chunya kwa Ujumla.
Hivi
karibuni kulifanyika zoezi la kuwaondoa wafugaji waliovamia msitu wa hifadhi
wa kijiji cha Mbangala ambapo Jumla ya mifugo 1000 ilikutwa msituni humo na
kufanyika uharibifu mkubwa lakini zoezi hilo liliingiliwa na hitilafu baada
ya wafugaji hao jamii ya Wamang’ati kuwashambulia kwa mishale na mikuki
maofisa pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi waliokimbia kunusuru maisha yao.
Na E
. Kamanga Chunya.
|
Home
News
WANAFUNZI ZAIDI YA 500 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI CHUNYA WASHINDWA KURIPOTI MASHULENI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment