Image
Image

EXCLUSIVE: CCBRT YAWATAKA WANAWAKE WENYE VIASHIRIA VYA FISTULA KUWAHI MAPEMA KUPATA TIBA.


Na. Salum Mkambala, Dar es Salaam.
Hospitali ya viungo ya CCBRT iliyopo jijini dar es salaam, imewataka wanawake wenye dalili au viashiria vya ugonjwa wa Fistula kwenda katika vituo vya afya na hospitali zingine zinazotibu ugonjwa huo mikoani kuchunguzwa kwanza badala ya kwenda moja kwa moja kwenye hospitali hiyo ili kuepusha mlundikano wa wagonjwa wasio na rufaa kutoka mikoani.

Mkurugenzi wa huduma za jamii wa hospitali ya CCBRT,  bi. Brenda Msangi ametoa wito huo jijini dar es salaam katika mahojiano maalumu juu ya  mwamko wa wagonjwa wa kujitokeza kupata huduma ya ugonjwa huo unaotajwa kusababisha ongezeko kubwa la wagonjwa wa fistula kwenye hospitali hiyo.
Brenda Msangi - Mkurugenzi wa huduma za jamii wa hospitali ya CCBRT 
Amesema kimsingi idadi ya wagonjwa wanaojitokeza kupata tiba imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na kampeni maalum ya mwezi mmoja iliyofadhiliwa na kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM na VODAFONE Foundation ijulikanayo kama Trasport my Patient ambayo wagonjwa hugharamiwa nauli na gharama za matibabu.

Hata hivyo amesisitiza kuwa licha ya CCBRT kutoa huduma hizo, bado huduma pia zimesogezwa na zinatolewa kwenye hospitali za mikoa na hata wilaya hivyo ili kupunguza usumbufu kwa wagonjwa kufuata huduma hizo mbali.

Takwimu zilizopatikana hospitalini hapo zinaonyesha kuwa zaidi ya wanawake 50 walifanyiwa upasuaji wa kutibu fistula kwenye hospitali hiyo ya CCBRT katika mwezi Mei mwaka huu pekee ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50 ya wanawake waliotibiwa kati ya Januari na Aprili mwaka huu ambapo malengo ni kuwatibu wanawake 650 kwa mwaka huu kutoka wanawake 501 waliofanyiwa upasuaji mwaka jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment