Image
Image

EXCLUSIVE: LITA ZA MAJI MILIONI MIATATU HADI MIASABA HAMSINI KUONGEZEKA KATIKA VITONGOJI NA JIJI LA DAR ES SALAAM.


Uzalishaji na usambaziji wa maji katika jiji la dsm na vitongoji vyake unatarajiwa kuongezeka kutoka lita milioni 300 hadi lita milioni 756  kwa siku kiwango ambacho ni mara mbili ya kinachozalishwa na kusambazwa sasa, ongezeko ambalo litatokana na kukalimika kwa mradi mkubwa wa kusambaza maji kutoka Ruvu hadi jijini dsm.

Mshauri mhandisi wa mradi wa ujenzi wa mabomba,  Rogers Mafuru amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani ambapo baada ya kukamilika unatarijiwa kuzalisha na kusambaza lita milioni 270 kwa siku ambapo pia bomba la zamani litaendelea kutoa lita 180 milioni kwa siku 
Rogers Mafuru - Mshauri mhandisi wa mradi wa ujenzi wa mabomba Amesema kazi inayoendelea sasa ni kusambaza mabomba ambapo katika maeneo mengi wananchi wametoa ushirikiano ikiwemo kukubaliana na kulipwa fidia ya maeneo yao ambako mradi huo unapita na kubainisha kuwa baadhi ya watu wanaendelea na mazungumzo na mamlaka ya maji safi na maji taka - DAWASA, ili kukamilisha taratibu za ulipaji fidia kuwezesha utekelezaji wa mradi huo.
Nelly Msuya - Meneja Uhusiano - DAWASA
John Moro - Diwani Kata ya Wazo.
Kwa mujibu wa DAWASA baada ya kukamilika kwa mradi huo upatikanaji wa maji katika jiji la dar es salaam utakuwa ni saa 24 tofauti na ilivyo sasa ambapo maji yanapatikana kwa saa nane tu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment