Image
Image

EXCLUSIVE: Nchi saba barani Afrika zapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa watoto: UNAIDS


Ripoti mpya kuhusu mipango ya kimataifa ya kupunguza na kumaliza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015 na kuwaongozea maisha mama zao imeonyesha hatua zilizopigwa katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto barani Afrika .
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa nchi saba zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zikiwemo Botswana , Ethiopia, Ghana, Malawi  na Afrika Kusini zimepunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto kwa asilimia 50 tangu mwaka 2009 huku mataifa mengine mawili Tanzania na zambia nayo yakipiga hatua. 

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kulikuwa na visa 130,000 vya maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto kwenye nchi hizo vikipungua kwa asilimia 38 tangu mwaka 2009.

 Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kupambana na ukinjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibe anasema kuwa hatua zilizopigwa kwenye nchi nyingi ni ishara tosha kuwa iwapo masuala muhimu yatazingatiwa watoto wanaweza kuzaliwa bila ya virusi vya ukimwi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment