Image
Image

EXCLUSIVE: JAMII YAASWA KUTO TUMIA DAWA ZA KULKEVYA.


Na Mwandishi wetu Faraja Kihongole aliyeko jijini Tanga 

Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya biashara za  dawa za kulevya baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya ambao wapo kwenye nyumba maalum ya mafunzo ya kuwasaidia kuachana na matumizi ya dawa hizo, wameitaka jamii kutothubutu kutumia dawa hizo kutokana na madharadhi  yake.


Mateja hao wanaoishi kwenye kituo kijulikanacho kwa jina la TANGA SOBER HOUSE, ambao wengine wameshatumia dawa hizo kwa zaidi ya miaka thelathini na wengine alishawahi kufanya kazi serikalini wanasema kutumia dawa za kulevya si ujanja na hakuna teja special, kwani madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya yanafanana kwa mateja wote na kwamba unapoanza kutumia madawa hayo ni sawa na kusimamisha maisha yako kwa sababu unakuwa huna uwezo tena wa kufikiria maendeleo ya maisha yako binafsi, familia, jamii na nchi kwa ujumla.
Ujumbe kutoka umoja wa mataifa ofisi ya tanzania umeendesha kongamano la vijana zaidi ya mia mbili mjini Tanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambayo hufanyika tarehe 26 June kila mwaka, na kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika mjini Dodoma.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment