Image
Image

EXCLUSIVE: JESHI LAPOLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHAMA CHA WANANCHI CUF.


Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na chama cha wananchi Cuf  kwenda ikulu siku ya ijumaa wiki hii kwa madai ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kulipangua jeshi la polisi pamoja na kutafutia ufumbuzi mgogoro wa gesi ya mtwara.

Kamishna wa polisi kanda maalum dsm CP SULEIMAN KOVA amesema maandamano hayo yamepigwa marufuku baada ya kupokea barua kutoka ikulu kuwa rais Kikwete hatakuwa na nafasi ya kupokea maandamano hayo kutokana na ujio wa marais watakaoshiriki mkutano wa Smart Partnaship Dialogue mwisho ni mwa wiki.
jeshi hilo pia limeonya wale wanaotakata kuaandaa mabango na maandamano wakati wa ujio wa rais wa marekani Barack Obama kwamba watachukuliwa hatua za kisheria, kufuatia taarifa za kuwepo kwa mpango huo.

Aidha katika kupambana na matukio ya uhalifu jeshi hilo limewatia mbaroni watuhumiwa wa ujambazi ishirini na wawili kati yao ni raia wa burundi  wakiwa na silaha nne aina ya SMG pamoja na bastola mbili zikiwa na risasi zaidi ya sitini. Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika operesheni maalum ambapo katika mapambano ya kurushiana risasi mmoja wa watuhumiwa alifariki dunia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment