Image
Image

EXCLUSIVE: SERIKALI YAWAHIMIZA WAZAZI, VIJANA NA WANANCHI KWA UJUMLA KUSHIRIKIANA KATIKA KUTOKOMEZA BIASHARA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KUTOKANA NA ATHARI ZAKE KWA JAMII NA TAIFA


Serikali imewahimiza wazazi, vijana na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanatokomeza biashara ya dawa za kulevya ndani ya jamii, kwa kuwa biashara hiyo haramu inaathari kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii pia.

Rai hiyo imetolewa mjini Dodoma na Waziri Mkuu bw. Mizengo Pinda katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Bw. William Lukuvi, katika maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya duniani.
Aidha, Waziri Mkuu amewaonya wale wote walio na mpango wa kuingia katika biashara hiyo, kutambua kuwa serikali ipo macho, na itawachukulia hatua za kisheria, huku wale watakaopatikana na hatia, watapata kifungo cha maisha.

Kwa upande wake,  Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Daw za Kulevya, Bw. Christopher Shekiondo, amesema kwa sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kilimo cha bangi, ambacho ndicho kinachochochea matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana.

Naye, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akapendekeza kutafutwa takwimu za wale wanaofanya biashara hiyo haramu, kama kweli watoto wao wanatumia dawa hizo, kwa kuwa madhara makubwa wanayaleta kwenye jamii.
Katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo Furahia Afya Yako na Si Dawa za Kulevya, vijana wawili, Robert Mbeho kutoka Dodoma na Nuru Salehe kutoka Zanzibar walitoa ushuhuda, jinsi dawa hizo zilivyotaka kuwapotezea ndoto zao.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment